Hatuendi kuabudu kwa sababu sisi tunataka, la! Bali ni amri na ni agizo la Mungu, kwa maana hiyo ili wewe uabudu unapaswa kuwa mtii katika hiyo amri, ukiabudu unaonyesha kuwa unamuheshimu Mungu na kumtii na hiyo inakuwa ni namna yako ya kuwasiliana na YEYE aliyekuumba.
Ibada ni namna ya kuwasiliana na yule ambaye ndiye chanzo chako, hivyo unapokwenda mbele za Mungu au kuabudu kuna vitu vingi unatakiwa kutafakari kabla haujaenda hapo, usiende kanisani kwa namna ulivyokuwa ukifanya, kwa sababu hauwezi kuabudu pasipo kuona muujiza wowote, Kwa namna unavyotii, namna yako ya kuabudu kwa Mungu ndivyo Mungu analeta watu kukuletea mahitaji yako, acha kulia usiku na mchana jifunze kuabudu kwa maana ukiabudu Mungu atafanya jambo kwako ili kukufanya wewe uwe na shukurani kwake. Ibada ni namna ya kuondokana na umasikini, Ibada ni njia ya kuelekea mafanikio, Ibada ni mahali ambapo utapata Baraka na ni mahali ambapo umefichwa, Unapoabudu Mungu anaweza kukufanya uwe namna anavyotaka uwe, ni lini utamtii Mungu wewe? Ni lini utajitiisha kwake?
OMBI:
Bwana yawezekana mimi ni mpumbavu, niondolee upumbavu wangu, kwa maana nataka niwe yule anatakayekupendeza wewe, yule ambaye unaweza kuwasiliana naye, nisaidie nataka nikupendeze wewe.
Dunia itapita na mambo yake yatapita lakini baada ya hayo yote liko pumziko. Kuna wakati inaweza kuonekana kama Mungu hayupo wala usaidizi haupo hata ukiita haitiki, ukiomba hakujibu, ukibisha hafungui, mambo yamebana kila kona; ukiangalia kushoto na kulia mambo yamebana, Wala hakuna usaidizi usikate tamaa Mungu yupo na wewe.
Angalia yale aliyokuvusha ni mengi sana na hata hilo linalokusumbua na lenyewe litapita, haijalishi nini kinatokea au nani anahusika lakini utapita katika hilo. Ayubu alipoteza kila kitu kwa muda wa miaka mitatu hana kitu chochote, akiwa na upele mwili mzima lakini alimtumaini Mungu kuwa yupo pamoja nae. Daudi alimkimbia mfalme kwa muda wa miaka kumi na tano, mfalme hakumpata kwa maana Bwana alikuwa pamoja naye; haikuwa ni kwa nguvu zake bali ni kwa nguvu za Bwana na wewe utapita katika hilo linalokusumbua, anayekuwinda hatakupata.
Sahau yaliyopita angalia yale amabyo Bwana anakwenda kufanya kwako. Yeye atakujulisha yaliopo, atabadilisha hata hayo yanayotaka kuja. Haijalishi ni mangapi umepitia lakini kuna Ushindi katika Yesu.
Kuna vitu unapaswa kuvifahamu ili uweze kumiliki:
1. Fahamu nafasi yako.
Mathayo 16:18 “Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.” Yapasa utajitambue wewe ni nani, wewe ni kanisa la Yesu Kristo umejengwa juu ya mwamba; kanisa ni nini? Ni nyumba ya Roho Mtakatifu, mahali ambapo Roho wa Mungu anamwabudu Mungu. Inamaanisha kua wewe ni kanisa. Na milango ya kuzimu ni kulizuia kanisa lisisonge mbele wala lisichanue.
1 Wakorintho 3:9 “Maana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu.” Tuna makundi matatu ya watu ndani ya kanisa,
• Watenda kazi pamoja na Mungu,
• shamba la Mungu ambao Mungu anawatumia ili kuzaa matunda, kuna wengine ndani ya kanisa awanatakiwa kuzaa matunda.
• Jengo, kuabudu yaani kumruhusu roho kuabudu. Je! Wewe uko wapi? elewa nafasi yako kwa Mungu wako.
Kanisa la Yesu Kristo limeamriwa kusonga mbele, hii inamaana kuwa wewe uliye mwamini umeamriwa kusonga mbele na siyo kukwama, yapaswa ukuwe, wewe ni kanisa la Yesu Kristo, kama jana ulikuwa na milioni moja leo yapasa uwe na milioni kumi na kesho yapaswa uwe na milioni mia, yaani kila siku kuwe na muendelezo kwako. Nakuamuru uende mbele kwa jina la Yesu na hakuna wa kukuzuia kwa jina la Yesu.
Mungu akujaalie kufahamu muda wa kutimiza jambo lako ambalo Mungu Amekukusudia, kila mtu ana muda wake wa kutimiza jambo lake, halijatimia kwako huenda umewahi sana au umechelewa. Mungu akupe kujua muda ufanye nini na wakati gani.