Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Neema

NENO LA SIKU.
Na Mtumishi Joshua Josephat Mwingira, Kanisa la Efatha.
Tarehe 16/11/2023.
Efe 2:8-10 “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu…..”
Nini maana ya Neema? Ni ile hali ambayo Mungu anakuwezesha wewe kuwepo mahali au kufanya jambo pasipokuwa na vigezo, yaani hauna sifa inayokufanya wewe kufanya hicho kitu lakini unafanya kwa sababu ya Neema. Katika Biblia tunamuona Mtume Paulo, yeye ndiye aliyechaguliwa kipindi ambacho Yesu alikuwa amekwisha kupaa, ina maana kuwa Paulo hakupata mafundisho ya Yesu alipokuwa duniani lakini Mtume huyu ndiye aliyeleta mabadiliko makubwa kuliko Mitume wengine. Katika Mitume waliofanya kazi kubwa Paulo ni mmojawapo. Katika kipindi cha utawala wa Rumi ilikuwa ni ngmu sana Injili kupenya lakini Paulo alihubiri, hakuangalia mazingira yanayo mzunguka bali aliangalia Neema aliyoibeba.
Paulo alikuwa anaua Watumishi wa Mungu, kwa maana hiyo hakukuwa na Mtume ambaye angeweza kumshuhudia habari za Yesu na akaacha yale ambayo alikuwa anafanya; hivyo Yesu akajitokeza Yeye mwenyewe kwa Paulo. Kutokana na kazi aliyoifanya Paulo ya kuua Watumishi wa Mungu kulikuwa hakuna msamaha kwa maana Mungu amesema “Anayegusa masihi wangu ni sawa na amegusa mboni ya jicho langu”. Lakini ilimbidi Yesu aje na kushusha Huruma na Neema yake kwanza kwa maana kama angemtaka Paulo atubu asingemaliza.
Unapokwenda kwa Mungu usianze kujieleza kuwa mimi nilifanya hiki na kile, Mungu hapendi maelezo mengi, Neema ya Wokovu inapokukuta itumie hiyo Neema vizuri. Mungu hapendi kutumia watu legelege hivyo usiangalie kule ulikotoka ukajihukumu sana na ukajiona hufai mbele za Bwana, Biblia inasema Ufalme wa Mungu unatekwa na wenye nguvu.
Kwako wewe uliyeokoka haijalishi watu wanakuonaje, haijalishi ulifanya maasi mangapi lakini Bwana amekurehemu na thamani yako mbele za Mungu ni kubwa kwa sababu una Neema ya tofauti. Neema inapatikana kwa wale ambao ni Wanyenyekevu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*