Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Nguvu ya kusikia

NENO LA SIKU.
Tarehe: 14/11/2023.
Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira.
Nguvu ya kufanikiwa inatokana na Kusikia, ndio maana Biblia inasema katika Kumbukumbu la Torati 28:1-2 “Itakuwa utakaposikia sauti ya BWANA, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo BWANA, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani; na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya BWANA, Mungu wako.”
Ukisikia ndipo utakuwa na uwezo wa kushinda kwa maana hauwezi kushinda kama haujasikia.
Batimayo kipofu baada ya kusikia habari za Yesu wa Nazareth ya kwamba Yeye ni Mponyaji, akaamua kumfuata ili aweze kuponywa, alipoamua kumwendea Yesu alipaza sauti yake, wanafunzi wa Yesu walipomnyamazisha Batimayo hakunyamaza, alipaza sauti yake ili aweze kupokea kile alichokisikia kutoka kwa Yesu. Ndipo Yesu alimuuliza “wataka nikufanyie nini?” Alisema nataka kuona na Yesu akampa kile alichokiomba.
Je! Wewe umesikia nini kuhusu habari za Yesu? Je! Umesikia Yesu ni Mponyaji? Mpaji, umesikia Yesu anaweza? Kile ulichokisikia na unachokitamani kutoka Kwake ndicho utakachokipokea. Kwa maana Mungu humpa kila atakaye haja yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*