Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

SEMINA YA UMILIKI – KANISA LA EFATHA MWENGE.

MCHUNGAJI JOSEPH SAFARI – KANISA LA EFATHA MWENGE.
Tangazo la kwanza limetoka kutoka kwa Baba yetu wa Mbinguni kupitia Mwanzo 1:28a “Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke,” hili ni tangazo la kwanza ambalo Mungu alilitangaza; Mungu anatoa baraka na baraka hizi zinaenda na mamlaka, nguvu na nafasi.
Mwanzo 1:28 “Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.” Katika maisha unayoishi umepewa kuzaa na kuongezeka. Kitu chochote ulichonacho lazima kiongezeke kwa maana maongezeko yameruhusiwa kwako, sasa kama wewe unamiliki duka likafa jua kuwa nguvu ya kumiliki imeondolewa kwako.
Kuzaa inamaana kuwa unamiliki kitu na lazima kile ulichonacho kiongezeke kisipoongeeka inamaana kuwa kuna nguvu yako ya kumiliki imekwisha chukuliwa. Huu ni wakati wako wa kumiliki muamuru yule aliyeiba nguvu yako ya kumiliki airejeshe mara saba.
Mwizi akiiba lazima akikamatwa arejeshe mara saba kwa maana Biblia inasema katika; Mithali 6:31 “ Lakini akipatikana, atalipa mara saba; Atatoa mali yote ya nyumba yake.” Chochote ulichoibiwa kwa muda mrefu huu ni wakati wako wa kumiliki mara saba, ikawe hivyo kwako kwa Jina la Yesu.
MAOMBI:
1. Omba Roho Mtakatifu akupe kuona Milki yako.
2. Muombe Mungu afungue macho yako uone milki yako ili uweze kumiliki.
UKIRI:
Akili yangu, nafsi yangu na mwili wangu kaa tayari kumiliki vile ambavyo Mungu amekuandalia kumiliki mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*