Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

SEMINA YA UMILIKI – KANISA LA EFATHA MWENGE: KUMILIKI NINI?

MCHUNGAJI LUCY MARTIN
Kumiliki ni kuwa na uhalali wa kuwa na vitu mbalimbali vilivyopo ardhini angani na kwenye maji. Hivyo basi kumiliki ni kuwa na mamlaka ya hivyo ulivyonavyo.
Tunaenda kumiliki wapi? Angani ardhini au majini, Vilivyo angani ardhini na majini ni vyako.
Tunaenda kumiliki kila kitamanikacho na kila kilicho chema kwa sababu Kristo ndiye aliyeviumba na ni vyakwetu.
Yakobo 1:17 “Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka.”
Kila kilicho chema kilichokamilika hushushwa kutoka juu; Bwana Yesu alikwisha kufa kwa ajili yetu hivyo tunauhalali wa kumiliki kwa sababu Bwana Yesu alishavilipia.
Zaburi 24:1 “ Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana, Dunia na wote wakaao ndani yake.” Huyu ambaye ni mmiliki wa hivyo vyote amekufia wewe ili uwe sehemu ya hivyo vyote.
Kwa nini tunamiliki?
1. Umiliki ni tabia ya Mungu, Mungu aliumba dunia hii ili kuiendeleza kumiliki na ikae chini ya uangalizi wa mwanadamu.
• Mimi na wewe tumeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu hivyo ile tabia ya Mungu ipo ndani yetu kwa maana kwa kadri baba alivyo ndivyo mwana alivyo, tunapaswa kumiliki.
2. Ni majira yetu kumiliki, sio kwa nguvu zetu bali yupo anayetuwezesha na Yeye anatupa kumiliki makubwa. Haya ni majira yetu kumiliki.
3. Ni sehemu ya baraka yako ambayo Mungu alikwisha kukuandalia.
Mungu aliyajua majira na nyakati na alijua kwamba 2024 ni mwaka wetu wa kumiliki; huu ni wakati na majira yako ya wewe kumiliki kwa maana ndio wakati sahihi ambao Mungu aliuandaa kwa ajili yako, chukua hatua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*