Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

SILAHA YA UTOAJI AU KUJITOA KATIKA NDOA.

NENO LA SIKU.
Na, Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira- Kanisa la Efatha.
Tarehe 23/07/2024.
Ili ndoa isiwe na udhaifu wowote, mume na mke wanapaswa kuwa Watoaji. Hii ina maana unapaswa ujitoe kwa mke wako/mume wako. Sio mume kila siku anakuletea zawadi na wewe mke hutoi zawadi kwa mume wako. Anaweza akakupa hela ukanunue nguo au mboga; ukiwa njiani unanunua mswaki unampelekea, ingawa hela amekupa yeye. Kuna wanawake wengine ni wabinafsi, wanajinunulia vitu vya kwao, hawakumbuki kuwanunulia zawadi waume zao.
Ifanye ndoa yako iwe hai na msababishe ibilisi akae mbali na ndoa yako.
Ibilisi ana akili sana ila unaweza ukamshinda kama ukivaa hii silaha, kazi ya kumshinda ibilisi ni rahisi.
Kama ibilisi akitamani kuharibu ndoa yangu, sitaomba kumwambia ibilisi ondoka katika ndoa yangu, la! Nitajitoa kwa mke wangu kwa sababu kwa jinsi ninavyojitoa ndivyo ninavyomwambia Mungu hiki ninakipenda hivyo Mungu atakilinda. Sio rahisi kwa ibilisi kuharibu kazi uliyoitaabikia kwa pendo kwa sababu Mungu ni Pendo. Kwa hiyo nikimtaabikia mke wangu kwa pendo, ibilisi hawezi kumuondoa kwangu kwa sababu nilichokifanya ni tendo la Mungu mwenyewe na ibilisi hawezi kuharibu tendo la Mungu.
Shetani hakimbii wala haummalizi kwa sababu umeomba sana, bali inategemea ni silaha ipi utakayotumia hiyo ndio itakayomuumiza shetani na kumuweka mbali na wewe.
Mwanangu, hekima ya Mungu ikupe kujua kitu gani kinampiga shetani ili asiharibu ndoa yako, biashara zako, kazi zako na familia yako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*