Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

SOMO: HAKI

NENO LA SIKU.

Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira- Kanisa la Efatha.

TAREHE 29/04/2024.

Haki ni kitu gani? Haki ni kuwa sahihi mbele za uwepo wa Mungu; Unafanyikaje kuwa sahihi?

1. Mpokee Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako, kuanzia hapo sio wewe tena unayeishi bali ni Yesu anaishi ndani yako na unakuwa mwana wa Mungu.

2. Timiza mapenzi ya Mungu na kusudi lake, usitumie muda kujaribu kurekebisha upumbavu wako mwenyewe maana kamwe hauwezi kufanikisha.

Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.”

Ikifika mahali ukajifunza kumtegemea Mungu, wewe sio mwenye dhambi tena au mjinga bali ni Mwenye Haki wa Mungu.

Mungu ndiye anayekupa Nguvu za kufanya yote kwa maana Yesu alichukua kushindwa kwako kote na kila kinachokufanya uwe mdogo; alichukua vyote na kukufanya Mtu Mkuu, wewe ni Hodari na Shujaa katika Yeye, unabeba Nguvu za Roho Mtakatifu, unaweza kusababisha wachawi wakimbie na umaskini usalimu amri, jidai katika Yeye.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*