Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

SOMO – MOYO WA IBADA.

MCHUNGAJI KIONGOZI; ANNA KOMBA
IBADA NI NINI?
Ibada Ni Maisha Ya Kumpa MUNGU Heshima Kuliko Chochote/Yoyote.
Ni Kumuonyesha MUNGU Pendo.
Tunajishusha Mbele Za MUNGU Nakuwa Mali Yake Yeye.
Hutakiwi Kuingia Na Heshima Yako Kwenye Ibada Bali Tunaingia Na Heshima Ya MUNGU.
Ibada Zipo Za Aina Nyingi Ikiwa Na Maaana Kwamba Wapo Wengi Wanaabudu Tu ili mradi Wameabudu Lakini MUNGU Yeye Anataka Watu Wanaomwabudu Yeye Katika Roho,Hiyo Ndiyo Ibada.
DALILI ZA WATU WENYE IBADA.
1.KUHESHIMU IBADA.
2.KUNYENYEKEA MBELE ZAKE.
3,KUTII MAAGIZO YAKE/SHERIA ZAKE.
4.KUMTEGEMEA MUNGU.
5.KUMTAMBUA MUNGU ANA NAFASI GANI KATIKA MAISHA YAKO.
6.KUWA MWAMINIFU MBELE ZA BWANA Daniel 3;1-18
Ili Ufanikiwe Kuabudu Lazima Uruhusu Moyo Wako Na Uelekeze Moyo Wako Kwa Bwana Yesu.
Mwanzo 2:16-17 Ili Adamu Aogope Ilitakiwa Amuheshimu MUNGU Na Kumtii Japo Alipokula lile Tunda Ndipo Kusudi La Adamu liliishia Pale Na Akafukuzwa Bustanini.
Mwanzo 4:4 Kuabudu Ni Pamoja Nakutambua Huyo Unaemuogopa Na Huyo Unaemuheshimu,Habil Na Kaini Walitoa Sadaka Ila Habili, MUNGU Aliridhia Dhabihu Ya Habili Kwasababu Alimtambua MUNGU Ana Nafasi Gani Kwake Na Alitoa Ile Dhabihu Kwa Kunyenyekea Na Hatimaye MUNGU Akazitakabali Sadaka Zake Ila Za Kaini Hakuzitakabali. MUNGU Anatafuta Watu Wenye Ibada, Walio Tayari Kutoa Kwa Moyo.
JE,UNATOA NINI UNAPOMUABUDU MUNGU?
Mwanzo 6:8-9 Nuhu Alikuwa Mwabudu Na Alikuwa Ana SIfa Zote Za Watu Wenye Ibada Kama Ibrahimu Na Kwa Hali Hiyo Nuhu Ndipo Alipopata Kibali Na Neema Machoni Pa BWANA.
Mwanzo 12:1 Ibrahimu Alikuwa Ni Mwabudu Kwahivyo Hata Muda Wake Wa Mungu alipomwambia “ toka katika nchi ya babako na jamaa zako Ulipofika Wala Hakuumuliza MUNGU Anaenda Wapi. Bali Alitii huo ndio moyo wa ibada!
Ukifanikiwa Kumtii MUNGU,Kunyenyekea,kumtambua Na Kumuogopa Basi Hapo Utakuwa Umefanikiwa,Kurudi Kwenye Ibada Ya Kweli Ina Maana Kwamba Urudi Kule Panapo Baraka Zako Na Neema Ile Ya Mwanzo.
KUNA AINA MBILI ZA IBADA
IBADA ZA AGANO LA KALE.
Waebrania 8:1-13
Tofauti Kati Ya Agano Kale Ilikuwa Kwenye Hema Na Kwenye Mlima Anaingia Mtu Ambae Ni Safi Hana Uchafu Wowote, Ina Maana Kwamba Agano La Kale Lilikuwa Lipo Kwaajili Ya Kuhukumu Ambao Walikuwa Wanafanya Dhambi Kipindi Hicho Walikuwa Wanauliwa. Ila Yesu kaja kutafuta na kuokoa kilichopotea. Ametusamehe! Labda wewe tu ujichanganye kwa kupenda ya nyuma kama mke wa Lutu!
IBADA ZA AGANO JIPYA
Yohana 4:21-24 MUNGU Ni ROHO Hivyo Anatafuta Wanaomwabudu Yeye Katika ROHO Na Kweli Hivyo Baada Ya Watu Kuzungumzia Yale Mambo Ya Agano La Kale,Musa Alifanikiwa Kumtoa MUNGU Mlimani Na Kumleta Hemani Yesu anamtoa amemtoa hemani na kumleta mioyoni mwetu. Hivyo MUNGU Akasamehe Kila Uovu Na Hatimaye Kukawa Na Agano Jipya linaloelezea Kuwa Watu Wamuabudu MUNGU Katika Pendo Na Katika Roho Na Kweli. Katika Roho Na Kweli ina Maana Kwa Moyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*