MWAKA WA KUMILIKI

MWAKA WA KUMILIKI
Mwaka wa kumiliki ni wa msingi sana katika maisha yako, kwa sababu ukiwa na kitu cha kumiliki utambulisho wako pia unakuwa mkuu. Kama hauna chochote cha kumiliki hata utambulisho wako unakuwa mdogo sana, hivyo namna unavyomiliki ndivyo unavyokuwa mkuu.
Kwa namna unavyo miliki ndivyo utambulisho wako unavyokuwa, hivyo umiliki ni kitu cha kurutubisha utambulisho wako, pasipo kuwa na kitu cha kumiliki ni rahisi kwako wewe kuwa mtu asiye na jina.
Umiliki unakusababisha uwe na hadhi; Mungu kamwe hajawahi kutembea na watu wasiojulikana, kuanzia mwanzo wa Biblia mpaka mwisho, Mungu alitembea na watu wanao tambulika, hivyo utambulisho pia ni muhimu sana katika mahusiano yako na Mungu.
Kwenye Biblia utakutana na mtu anayeitwa Eliya, anaonekana kama ni mtu asiye na jina kwa sababu hatujaona alipoanzia lakini tunaona tu akitembea na Mungu, maana yake ni kuwa Mungu alimjua tangu mwanzo. Eliya alikuwa anamiliki kitu cha kipekee ambacho hakikujulikana kwa wanadamu ila kwa Mungu, hivyo umiliki wako ni wa msingi sana kwa ajili yako ili kuumba mazingira ya mahusiano na Mungu.
© MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA

Add Comment