Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

TAMBUA MAMLAKA YAKO ULIYOPEWA NA MUNGU ILI UWE MSHINDI.

NENO LA SIKU.
Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira – Kanisa la Efatha.
Tarehe 24/1//2024.
Luka 10:19 “Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.”
Yesu alisema hilo baada ya kuwatuma wanafunzi wake kufanyia kazi Mamlaka aliyowapa, aliwatuma kuonyesha Mamlaka yao juu ya nyoka, nge na mapepo, waliporejea walimpa ushuhuda wa kilichotokea.
Sisi ni waaminio (tuliookoka) tunapaswa kutumia Mamlaka yetu tuliyopewa bila wasi wasi, tunayo Mamlaka lakini haiwezi kutenda kazi mpaka tujue namna ya kuwasiliana na Yule aliyetupa hiyo Mamlaka, kwa maana sisi tunayo Mamlaka lakini Yeye anao uwezo wa kusababisha vitu vitokee. Biblia ni kitabu ambacho kitakufundisha na kukufanya ufanyie kazi Mamlaka yako.
Unapotendea kazi Mamlaka yako ndipo Mungu anaachilia Nguvu na uwezo wa kuhakikisha kile unachokitaka kiwe. Wewe mwaminio unayo Mamlaka juu ya mazingira yako, maisha yako na familia yako usiishi kama mkimbizi, jua nafasi yako kwa maana unapotambua nafasi yako ndipo unaweza kuitambua Nafasi ya Mungu kwako na kuanzia hapo ushindi ni wa kwako.
Wewe uliyeokoka ukiitambua Mamlaka ambayo Mungu amekupa na ukaitendea kazi ndipo maisha yako yataleta maana hapa duniani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*