Tenda kwa ushujaa na uhodari ili upate kumiliki

NENO LA SIKU
Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Kanisa la Efatha
Tarehe 17/10/2024
Yoshua 1:7 “Uwe hodari tu na ushujaa mwingi, uangalie kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kuume, au wa kushoto, upate kufanikiwa sana kila uendako.”
Mafanikio hutokana na Juhudi katika Kazi. Mtu anapofuata maelekezo ya kufanya mambo ili yapate kutokea huingia katika hatua ya Ustawi, asipotenda kwa Ushujaa na Uhodari hawezi kustawi.
Mungu alimwagiza Yoshua awe Hodari na Moyo wa Ushujaa ndipo ataweza kuwarithisha Wana wa Israeli Nchi yao ya Ahadi, hii inamaana kuwa kama asingekuwa hodari na mwenye moyo wa ushujaa asingewarithisha wana wa Israel nchi ya ahadi.
Unavyojihurumia nakuacha kufanya kitu kwa Mungu unakuwa mbali na Baraka zako. Neno linasema katika Zaburi 126:5 “Wapandao kwa machozi watavuna kwa kelele za furaha.”
Je! Unataka kumiliki milki zako? Acha uvivu, ni kweli tumetangaziwa huu ni mwaka wa kumiliki lakini usifikiri kwa wewe kuendelea kukaa na kuimba mwaka wa umiliki utamiliki kitu, la! Inuka na ufanye kitu huku ukimuomba Mungu akufanikishe ndipo utaona akikubariki na hata kufikia kumiliki yale unayoyataka.

Add Comment