Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Ujionavyo nafsini ndivyo ulivyo

NENO LA SIKU.
Tarehe: 30/10/2023.
Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira.
Zaburi 103:1 “Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA. Naam, vyote vilivyo ndani yangu Vilihimidi Jina lake takatifu.”
Uwezo na ushindi wa mafanikio yako, utategemea sana ndani yako kuna nini; Neno la Mungu linasema “Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA. Naam, vyote vilivyo ndani yangu vilihimidi Jina lake takatifu.” Kwa nini haufanikiwi? Shida sio changamoto unazopitia, matatizo yanayokukuta au mumeo/ mke wako, la! Bali ni ndani yako ndiko kuna shida. Ndani yako kunatoa nini? Huwa unaongea nini wewe? Unajionaje? Kwa maana Biblia inasema “ajionavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo,” jinsi unavyojiona ndani yako ndivyo ulivyo. Ukijiona maskini, uliyeshindwa, mbaya ndivyo utakavyokuwa.
Biblia inasema, “eeh nafsi yangu umhimidi BWANA” unapomhimidi BWANA kutoka ndani yako ndipo huyo aliyeko ndani yako anainuka na kukufanya kuwa Mkubwa.
Kwa kadri unavyowaza na kuhisi kutoka ndani yako basi hivyo ndivyo ulivyo, kwa maana hayo unayoyawaza ndiyo utakayoyanena na kuyatenda. Shida sio yule mwanaume anayekusumbua au mkeo mwenye kelele; bali shida ni wewe, Je! ndani yako unawaza nini ? Ili ufanikiwe katika maisha yako badili kwanza namna ya kuwaza au kufikiri kwako, mara zote waza mambo makubwa unayotaka katika maisha yako nayo yatakuwa ya kwako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*