Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Ujumbe wa Mungu kwa wazaliwa wa mwezi wa kumi na moja.

NENO LA SIKU.
Tarehe: 1/11/2023.
Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira.
Isaya 43:4-7 “Kwa kuwa ulikuwa wa thamani machoni pangu, na mwenye kuheshimiwa, nami nimekupenda; kwa sababu hiyo nitatoa watu kwa ajili yako; na kabila za watu kwa ajili ya maisha yako. Usiogope; maana mimi ni pamoja nawe; nitaleta wazao wako toka mashariki, nitakukusanya toka magharibi; nitaiambia kaskazi, Toa; nayo kusi, Usizuie; waleteni wana wangu kutoka mbali, na binti zangu kutoka miisho ya dunia. Kila mmoja aliyeitwa kwa Jina langu, niliyemwumba kwa ajili ya utukufu wangu; mimi nimemwumba, naam, mimi nimemfanya.”
Wazaliwa wa mwezi wa kumi na moja ninyi ni kizazi cha sherehe, kwa maana hata ukiwaudhi Mungu anawaletea kufurahi. Wamezaliwa ili wafurahi, Mungu hawanyimi chochote cha kula, wanakula vizuri mno. Huwa hawajui kuangalia kesho, wakiwa wana chakula hawajizuii kula wanakula chote na hata kama wakila chote lakini Mungu anawapa tena; kwao hakuna kupungukiwa.
Ni wachache sana wazaliwa wa mwezi huu utawakuta wamekonda, asilimia kubwa wana afya nzuri.
Ewe mzaliwa wa mwezi huu yakupasa umshukuru Mungu na umuombe akupe kuziona Baraka zote alizokukusudia katika maisha yako sawa sawa na Mwezi wako wa kuzaliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*