Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

UMECHAGULIWA.

NENO LA SIKU.
Tarehe: 15/04/2024.
Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira.
Isaya 43:4 “Kwa kuwa ulikuwa wa thamani machoni pangu, na mwenye kuheshimiwa, nami nimekupenda; kwa sababu hiyo nitatoa watu kwa ajili yako; na kabila za watu kwa ajili ya maisha yako.”
Usiangalie mabaya uliyopitia wala mtu asikusumbue na yaliyopita, bali songa mbele chuchumilia thawabu ya mwito mkuu wa Mungu.
Wewe uliyeokoka unatakiwa ujue kuwa UMECHAGULIWA NA BWANA. Watu hufikiri kuwa, uliokoka kwa sababu ulipatwa na matatizo, ulikuwa mgonjwa au ulishuhudiwa. Ukweli ni kwamba UMECHAGULIWA na Mungu. Kuchaguliwa ni matakwa ya yule anayechagua na sio matakwa ya anayechaguliwa.
Bwana Yesu alitumia kila njia ili akupate, kwa wengine alitumia mapepo, wengine magonjwa, wengine kipigo cha waume zao, wengine makandamizo ya wakwe na kadhalika. Wewe ni Wathamani sana, usijidharau wala KUDHARAULIWA NA MTU mwingine kwa hali yoyote, watu wanaweza kukubeza kwa kila hali na kukuona hujaokoka. Jibu lako liwe ninachokijua ni kuwa Bwana YESU alikuja ili NIWE WAKE, tena hana ubaguzi.
Mwana wa Mungu, wewe uliyeokoka jua kuwa umechaguliwa na kama umechaguliwa ina maana kuwa wewe ni wa thamani sana mbele za BABA yako wa Mbinguni; hivyo tunza Wokovu wako kuliko chochote uwezacho kutunza. Usiyatazame yale unayopitia sasa hata ukakata tamaa, bali unapaswa kutambua kuwa, aliyekuchagua hatakuacha kamwe, endelea kumwamini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*