Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Unahitaji Nguvu za Mungu ili uweze kuamrisha yale yaliyokamatwa na ibilisi ili yapate kukujilia.

NENO LA SIKU.
Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Kanisa la Efatha.
Tarehe 25/11/2023.
Warumi 8:37 “Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.” Katika Yeye tunashinda mambo yote na sio moja.
Unapoanza mpambano wako na ibilisi, cha kwanza ni kutengeneza na Mungu wako kisha ndipo unatafuta Nguvu zake ili uweze kuyashinda mawazo na nguvu za ibilisi. Ibilisi anatukandamiza katika roho lakini matokeo yake tunayaona katika mwili, hivyo ili umshinde unapaswa kuwa rohoni.
2 Wakorintho 10:3-5 “Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;) tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikra ipate kumtii Kristo;” Hatushindi kwa sababu tuna nguvu za kimwili, la! bali kwa sababu ya Nguvu ya rohoni.
Unahitaji Nguvu za Mungu ndani yako ili uamrishe yale yaliyokamatwa na ibilisi ili yapate kukujilia.
• Biblia inasema “maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome” Kichwani kwako kuna ngome iliyojengwa na adui ili usije ukaruhusu mawazo ya Mungu kuingia kwako na kukubadilisha.
• “Tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu” wakati wewe unaambiwa unapendwa na Mungu anakwenda kukubariki ibilisi anainuka kwako na kuanza kukwambia, we nani aliyewahi kukupenda au nyumbani kwenu ni nani aliwahi kumiliki nyumba nzuri? Kwa hiyo akilini mwako kunajaa mawazo mabaya mwisho wa siku unarudi nyuma na kufikiri kuwa hauwezi.
Ili uweze kushinda hiyo akili na mawazo ya ibilisi kwako unapaswa kuwa na Nguvu ya Mungu ambayo itakuwezesha wewe kushinda.
Elimu yoyote iliyojengwa kinyume na mawazo ya Mungu katika akili yako hiyo ni ngome kwako, sasa ili uweze kuishinda ni lazima ubomoe hiyo ngome, unaibomoaje? Kwa wewe kulijua Neno la Mungu kwa wingi ndani yako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*