Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

USHUHUDA:

Anaitwa Sheyla Shihoza, anapenda kumshukuru Mungu kwa matendo yake makuu aliyomtendea, alikaa katika gereza la Segerea kwa muda wa miaka 3 akiwa anasubiri hukumu ya kesi iliyokuwa ikimkabili ya utatatishaji fedha (kesi ya kuhujumu uchumi). Wakati yupo katika gereza la Segerea alipoteza matumaini ya kutoka kabisa kulingana na kesi iliyokuwa ikimkabili.

Sheyla anasema baada ya kukosa tumaini akaamua kumkimbilia Yesu na baada ya kuokoka akiwa gerezani akaanza kuuona usaidizi wa Mungu katika maisha yake.

Sheyla anasema pia alikuwa anasumbuliwa na maradhi mbalimbali na uvimbe kwenye kizazi ila anamshukuru Mungu kwa ajili ya wachungaji wa Efatha wanaohudumia wafungwa kule gerezani, Mungu awabariki sana maana kupitia wao ameweza kumjua Mungu na sasa ameokoka.

Sheyla anasema ameona mkono wa Mungu katika maisha yake na hakika hatamuacha siku zote za maisha yake, atamtumikia maana aliyofanya kwake ni makubwa sana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*