Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

USHUHUDA: AMEPANDA CHEO SASA NI PROFESSOR

USHUHUDA.

Naitwa Prof. Emmanuel Chao, ninapenda kumshukuru sana Mungu kwa kupanda cheo. Kuna mambo mengi ambayo Mungu amefanya katika maisha yangu ambayo sikuwahi kufikiri wala kuwaza, mara nyingi sana nilipokuwa nikisalimiana na Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira alikuwa akiniita Professa, na ndani yangu nilikuwa najisikia kuwa hivyo ndipo nikaamua kutuma maombi kwa ajili ya hicho cheo. Haikuwa rahisi sana kuipata hiyo nafasi tena ukiwa na umri fulani, lakini mimi niliamua kutuma maombi nilijua kuwa ni jambo ambalo halijawahi kutokea lakini niliamua kutuma maombi nikiamini kuwa Mungu wangu ni Mungu ambaye anaweza kutengeneza njia mahali pasipo na njia.

Mwaka huu ulipoanza nikamwambia Mungu huu ni mwaka wa kumiliki na mimi nataka kumiliki yale maono ambayo niliyoyatarajia. Kwa mara ya kwanza niliona jambo la ajabu sana kwani watu waliokuwa wanahusika na huo mchakato wa kupokea maombi waliungana ili kuhakikisha ombi langu linafanikiwa. Baada ya kuwasilisha maombi ndani yangu nilihisi furaha na nilijua ya kwamba mwaka huu wa kumiliki Bwana ananipa kumiliki kile nilichotarajia, na ilipofika tarehe 16 mwezi huu nimefanikiwa kutangazwa kuwa Professor na sio tu nimepanda cheo lakini pia nimekuwa na alama za juu sana kuliko wote waliopanda katika hiyo nafasi. Nina kila sababu ya kumshukuru sana Mungu kwa kuniwezesha lakini pia namshukuru sana Mungu kwa ajili ya wazazi wangu wa kiroho na wazazi wangu wa kunizaa wamekuwa pamoja nami katika wakati wote. Katika maisha yangu wakati wote nimekuwa nikiipa kazi ya Mungu kipaumbele, ninaamini kuwa si kwa nguvu zangu wala uweza wangu bali ni kwa uweza wa Mungu amefanikisha haya sifa na utukufu namrudishia Baba yangu wa mbinguni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*