Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira
Yohana 14 “Yesu akawaambia, “Msifadhaike mioyoni mwenu. Mwaminini Mungu, niaminini na mimi pia. Katika nyumba ya Baba yangu mna nafasi nyingi. Kama sivyo, nisingeliwaambia kwamba nakwenda kuwaandalia makao. Na nikishawaandalia, nitarudi kuwachukua mkae pamoja nami; ili mahali nilipo, nanyi mpate kuwepo. Ninyi mnajua njia ya kufikia ninakokwenda.”
Tomaso akamuuliza, “Bwana, hatujui unakokwenda; tutaijuaje njia? Yesu akawaambia, “Mimi ndiye Njia na Kweli na Uzima; mtu hawezi kufika kwa Baba bila kupitia kwangu. Kama mngekuwa mnajua mimi ni nani, mngemfahamu na Baba yangu. Tangu sasa mnamfahamu Baba yangu na mmemwona.”
Huwezi kuiona mbingu pasipo kupita kwa Yesu, hakuna njia yoyote ya kuingia Mbinguni bila kumjua Yesu Kristo, haijalishi wewe ni Mkristo, mpagani au una dini yoyote ile, ila njia ya kufika kwa Baba (Mbinguni) ni moja tu; ni Yesu Kristo, Yeye aliyekufa pale msalabani kwa ajili ya watu wote ili kwa kupitia kifo chake tupate kumuona Baba wa mbinguni.
Yohana 1:12 “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio Jina lake.” Kwa kupitia kifo cha Yesu pale msalabani tulifanywa kuwa wana wa Mungu.
Amosi 3:3 “Je! Watu wawili wanaweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana?” Kwako wewe uliyeokoka, Je! Umefanyika kuwa mwana? Je! Unatii yale maagizo yote unayoagizwa wewe kama mwana? Je! Unamtii anayekuongoza na umepatana naye? Lazima upatane na yule aliyetumwa kukuongoza ili uweze kuziona baraka zako.